Ndugu
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Napenda
nichukue fursa hii kuwajulisha rasmi kwamba Nchi yetu imepata heshima ya
kutembelewa na Waziri Mkuu wa Thailand ambaye atawasili Nchini tarehe
30/07/2013.
Ziara hii ni ya kikazi (state visit) na atawasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere majira ya
saa 6:30 mchana na kulakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais wetu mpendwa Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete akifuatana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa.
Ndugu
Wananchi, Baada
ya kuwasili Mhe. Waziri Mkuu wa Thailand atakagua gwaride maalum lililoandaliwa
kwa ajili yake na pia atapata fursa ya kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma
ambavyo vitakuwa vikitumbuiza na kutoa burudani kwa Mgeni wetu na msafara wake.
Ndugu
Wananchi, Mgeni
wetu baada ya kukagua vikundi vya ngoma na burudani ataondoka kuelekea Ikulu
kupitia barabara ya Nyerere, Railway, Gerezani, Sokoine Drive hadi Ikulu. Akiwa
Ikulu atasaini mikataba mbalimbali kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand.
Usiku atashiriki katika dhifa maalumu iliyoandaliwa na Mwenyeji wake.
Ndugu
Wananchi, Tunaomba
radhi kwamba barabara hizi nilizozitaja zitafungwa kwa muda kupisha misafara ya
Viongozi wetu Wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Kumbukumbu ya
Mwalimu J. K. Nyerere kumlaki Mgeni wetu hususan barabara ya Nyerere kuanzia
saa 6.00 mchana hadi saa 7.30 mchana.
Ndugu
Wananchi, Tarehe
31/07/2013 Waziri Mkuu wa Thailand atatembelea Mbuga za Wanyama za
Serengeti.Tarehe 01/08/2013 atarejea Dar es Salaam na kuagwa rasmi katika
Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere na kuendelea na ziara yake huko Uganda.
Ndugu
Wananchi, Kama
ilivyo ada tunaombwa kumlaki mgeni wetu kwa shangwe na bashasha katika maeneo
yote atakayopita.
Asanteni
kwa kunisikiliza.
Saidi Meck Sadiki
MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment