Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi
wa kwanza wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw.
Mohamed Ramadhani Mnjori (39) muuz nguo za mitumba, mkazi wa Ilala – Dar es
Salaam kwenye halfla ya makabidhiano iliyofanyika eneo la Soko Kuu la Kariakoo,
Dar es Salaam.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kushoto)
akimpa mkono wa pongezi mshindi wa kwanza wa promosheni ya ‘Miliki Biashara
Yako’ ibuka na Bajaji Bw. Mohamed Ramadhani Mnjori (39) alipopanda kukagua
Bajaji yake. Bajaji hiyo ina thamani ya Tsh 6,700,000.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia)
akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa pili wa promosheni ya ‘Miliki Biashara
Yako’, Bw. Riziki Lucas
Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam. Tigo
tayari imelipia leseni ya barabani (Road license) na bima kwa ajili ya Bajaji
hizo.
Anachotakiwa mteja sasa, ni kuanza biashara yake bila shida mara moja. Mshindi huyu aliwaacha watu hoi pale aliposema kazi zake ni ngumu mno. Hivyo kwa kupata bajaj sasa mambo yake yatakuwa mazuri.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga
akimtambulisha mshindi wa tatu wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Adam Saidi Kalulu (36) mkulima, mkazi wa Kiluvya kabla
ya kumkambidhi Bajaji yake mpya mbele ya wanahabari na wananchi waliojitokeza
eneo la Soko Kuu la Kariakoo kushudia makabidhiano hayo.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (mwenye
kofia ya Tigo) katika picha ya pamoja na washindi watatu wa kwanza ya promosheni
ya ‘Miliki Biashara Yako’ ibuka na Bajaji wakati wa sherehe ya makabidhiano
iliyofanyika leo eneo la Soko Kuu, Kariakoo. Mteja wa Tigo anao uwezo wa
kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh
1,000 tu kwa siku.
Mshindi wa pili wa promosheni ya ‘Miliki
Biashara Yako’, Bw.
Riziki Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es
Salaam akitoa ushuhuda mbele ya vyombo vya habari jinsi hapo zamani alipokuwa
akihangaika na kazi ‘ngumu ngumu’ ambazo zilikuwa hazimpi kipato cha kutosha
cha kuendeshea maisha yake. Mshindi huyo ametoa shukurani nyingi sana kwa Tigo
na ametoa rai kwa watanzania wengine waweze kushiriki. “Hakika Tigo
imebadilisha maisha yangu,” Riziki alisema. Pembeni yake ni Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga.
Bajaji 3 kati ya Bajaji 60
zilizoshindwa na washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Miliki Biashara
Yako’ zikipaki eneo la Soko Kuu, Kariakoo kabla ya kukabidhiwa kwa washindi
mapema leo. Zimebakia Bajaji 57 zakushindaniwa, droo inayofuata itachezwa siku
ya Jumatatu 29 Julai, 2013 kwa ajili ya kuwapata washindi 7 wa wiki hii. Wateja
wanaweza kuendelea kushiriki kwa kuongeza salio mara nyingi wawezavyo ili
kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji na kumiliki biashara zao
wenyewe.
No comments:
Post a Comment