Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KITUO cha watoto
yatima cha Yatima Islamic, kinaomba msaada kwa wasamaria wema kukisaidia pango
la nyumba.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kituo hicho kilichopo
Buguruni Ally Hamza, Rashid Akungwa alisema kuwa, wanadaiwa pango zaidi ya sh.
milioni nne, baada ya awali waliyolipiwa na mhisani kuisha muda wake.
"Awali
alijitokeza mtu ambaye, aliona mazingira ya watoto, kwamba tulikuwa katika nyumba
ya vyumba viwili, na watoto ni wengi..ndipo alipotutafutia sehemu hii na kutulipia
kodi ya mwaka ambayo imeshamalizika tangu mwezi uliopita,"aliongeza.
Alisema
kwa sasa wana hali mbaya, na endapo watafukuzwa katika nyumba hiyo, basi watoto
hao zaidi ya 50, huenda wakakosa pa kwenda na hatimaye kuzagaa mitaani.
Watoto
wengi wanaoishi katika kituo hicho wana umri kati ya miaka minne hadi 15, ambapo
wengi wanasoma shule ya msingi, huku mmoja aliyekuwa akisoma sekondari,
amemaliza.
Katibu
wa kituo hicho, Aboubakary Simba, alisema mahitaji mengine ni pamoja na futari
na daku hasa kwa mwezi huu wa Ramadhani, mavazi kwa ajili ya watoto na mahitaji
ya kawaida ya kibinadamu.
Alisema
msaada wa aina yeyote wenye hadhi na utu, unapokelewa na kwa yeyote ataliyeguswa
kuchangia anaweza kupata maelezo kupitia namba 071 03 8888 au 0712150928.
No comments:
Post a Comment