Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
RAIS wa Marekani, Barack Obama, ameondoka
muda mchache kuelekea nyumbani kwao, huku akiacha historia katika mataifa haya
mawili, Tanzania na Marekani.
Kwaheri na karibu tena Tanzania Rais Barack Obama.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barack Obama wa Marekani aliyeondoka leo kurudi nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku za mbili nchini hapa.
Akiwa Uwanja wa Ndege, Obama ameagwa na
Rais Jakaya Mrisho Kikwetee, ambaye ndio mwenyeji wake na kuacha ardhi ya
Tanzania iliyomlaki kwa furaha za aina yake.
Gari la Barack Obama likiwa na walinzi.
Tangu jana alipowasili, Rais Obama alikuwa
ni mwenye furaha tele moyoni mwake, huku saa zote akiachia tababu lake, sanjari
na mke wake, Michelle aliyeambatana na watoto wao wawili.
Kubwa la kusisimua ni namna gani ulinzi
uliimarishwa kwa ajili ya kuhakikisha Obama anakuja na kuondoka salama, wakati
ujio wake haukupokewa kwa shangwe na Wakenya, wakiwamo wafanyabiashara wao
wawili waliosusia mwaliko wa kukutana na Obama kujadili mambo ya kibiashara.
Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege,
akitokea Ubungo alipokwenda kuangalia shughuli za ufuaji wa Umeme kutoka
Kampuni ya Symbion, Obama na Kikwete waliangalia ngoma za vikundi mbalimbali
vilivyompa burudani ya aina yake.
Rais Obama aliwasili jana Tanzania katika
ziara ya siku mbili ya kikazi, ambapo pia ujio wake ulitokea nchini Afrika
Kusini baada ya kutokea pia nchini Senegal.
Sera kubwa aliyojivunia Obama na Kikwete
katika ziara yao ni kuhakikisha kuwa Afrika na Tanzania kwa ujumla inatumia
vyema program za umeme kwa ajili ya maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment