Na Boniface Wambura, Uganda
Taifa
Stars imewasili salama hapa Kampala tayari kwa mechi ya marudiano ya
mchujo dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani
nchini Afrika Kusini.
Mrisho Ngassa, nyota wa Taifa Stars
Stars
ambayo iliwasili ikitokea jijini Mwanza ilipokuwa imepiga kambi ya siku
kumi kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo
mbili itakwenda Afrika Kusini mwakani imefikia hoteli ya Mt. Zion
iliyoko eneo la Kisseka katikati ya Jiji la Kampala.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Kim
Poulsen ameridhishwa na kiwango cha hoteli hiyo, kwani ndiyo ambayo timu
ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) ilifikia Novemba mwaka jana
ilipokuja Kampala kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa
na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Stars
ambayo ilitiwa chachu na Rais Jakaya Kikwete alipokutana nayo Uwanja wa
Ndege wa Mwanza wakati ikiondoka kuja Kampala, na kuitakia kila la
kheri itafanya mazoezi yake ya mwisho kesho (Julai 26 mwaka huu) Uwanja
wa Mandela kujiandaa kwa mechi ya Jumamosi.
Kocha
Kim amesema ingawa mechi hiyo ni ngumu, lakini kikosi chake kimejiandaa
kuikabili Uganda kwani wachezaji wako wako vizuri na ari kwa ajili ya
mechi iko juu.
Wachezaji
wote wako katika hali nzuri, isipokuwa Khamis Mcha aliyekuwa na maumivu
ya goti, lakini kwa mujibu wa madaktari wa timu anaendelea vizuri kwani
tayari wanampa mazoezi mepesi.
Kikosi
cha kamili cha Stars ilichoko hapa kinaundwa na makipa Juma Kaseja,
Mwadini Ali na Ali Mustafa. Mabeki ni Aggrey Morris, David Luhende,
Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir Haroub na Vincent Barnabas.
Viungo
ni Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis
Mcha, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni
John Boko, Juma Luizio na Mrisho Ngasa.
No comments:
Post a Comment