Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU
ya Yanga, leo itaaondoka mkoani Shinyanga na kuelekea mkoani Tabora kwa ajili
ya kuendeleaa na ziara yao na kuwatembelea wadau na mashabiki wao mkoani humo.
Wakiwa
huko, timu ya Yanga itaendelea na mazoezi yake sambamba na kucheza mechi za
kirafiki na timu kadhaa mkoani Tabora.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto
Akizungumza
jana kwa njia ya simu, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kuwa baada
ya kutoka mkoani Mwanza na kutua Shinyanga, wameona waelekee Tabora kabla ya
kupanga safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Alisema
ziara hiyo ni sehemu ya kujiandaa na ligi ya Tanzania Bara, wakiamini kuwa pia
utakuwa utaratibu mzuri wa kurudisha fadhira kwa mashabiki wao.
“Bado
tutaendelea kuwa mikoani, maana kesho (leo) msafara wetu utaelekea mkoani
Tabora ambapo huko tutacheza mechi ya kirafiki na timu ambayo bado hatujaijua.
“Ziara
hii ipo kwa ajili ya kuwatembelea mashabiki wetu kwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga
na Tabora, ikiwa ni kawaida kwetu Yanga,” alisema.
Ligi
ya Tanzania Bara ambapo Yanga ndio bingwa mtetezi wake inatarajia kuanza
kutimua vumbi mwezi ujao, huku timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo
zikiendelea na mazoezi ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa patashika hiyo.
No comments:
Post a Comment