KODI ya
simu ya shilingi 1000 kwa mwezi, imeendelea kuwa Habari tata kwa Watanzania, huku viongozi wa serikali,
wakiwamo wabunge kusimama kidete kuipigania ili iondolewe na kuwafanya wananchi
waishi vizuri, huku serikali ikifikiria namna ya kuiondoa.
Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, pichani
Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, kwa siku kadhaa sasa amekuwa
akirushiana maneno katika mitandao na baadhi ya wabunge wa Chadema, akiwamo
John Mnyika, mbunge wa Ubungo.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba
“Sikubaliani
na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa nguvu. Lakini najua haliwezi
likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza
kodi.”
Makamba
alisema kuwa wabunge hao ni wanafiki maana wenyewe walikubali ipitishwe, ingawa
kwa sasa wameonekana kushikia bango kwa ajili ya kuomba huruma kwa wananchi.
Waziri wa
Fedha, Dk William Mgimwa, aliizungumzia katika vyombo vya Habari kuwa suala hilo linaangaliwa upya na
ikiwezekana itafutwa ili kusitisha mgogoro kutoka kwa wadau wa mawasiliano.
Alisema
msimamo wa wizara yake katika suala hilo
ni tofauti kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za mawasiliano
zinapungua... “Wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu ni kupunguza gharama
za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.
“Nia yetu
ni kushusha gharama iwe sifuri kabisa, kitu chochote kinachopandishwa bei sisi
hatukubaliani nacho kwa kuwa ni kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini.
Bidhaa ambayo inatakiwa kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo,” alisema
Mgimwa.
No comments:
Post a Comment