Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
BONDIA wa ngumi za
kulipwa hapa nchini, Mbwana Matumla, amesema kwamba Tanzania bado inaandamwa na
ukosefu wa mapromota, hali inayosababisha mchezo wa ngumi usifanye vizuri
zaidi.
Bondia Mbwana Matumla, pichani.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Matumla alisema kuwa uhaba huo wa mapromota kunasababisha
mabondia wengi washindwe kupata nafasi ya kuonyesha makali yao ulingoni.
Alisema endapo
mapromota wangekuwa wengi, hata mwamko katika mchezo huo ungekuwa mkubwa, hivyo
kuwafanya mabondia wapya kutamani zaidi tasnia hiyo ya masumbwi.
Matumla aliendelea
kusema wapo mabondia ambao kwa mwaka wanapanda ulingoni mara moja au wasipande
kabisa katika kuwania mikanda mbalimbali, hivyo kuathiri vipaji vyao.
“Kama bondia anakosa
pambano, ina maana kipaji chake kinaweza kupotea, ukizingatia kuwa kabla ya
kuangalia nje ya nchi lazima awe na rekodi nzuri katika mapambano ya ndani.
“Hali hii
inasababisha wadau wa ngumi waone kuna haja sasa ya kuingia katika mchezo wa
masumbwi kwa ajili ya kuuweka juu zaidi kwa kuhakikisha kuwa wanaandaa
mapambano,” alisema Matumla.
Matumla anayetokea
katika familia wana masumbwi ni miongoni mwa mabondia wenye uwezo wa juu katika
mchezo huo, huku akifanikiwa kuibuka na ushindi katika mapambano mengi
anayopanda ulingoni.
No comments:
Post a Comment