Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
ALIYEKUWA mgombea udiwani wa
Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni mkoani Tanga, kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Mwamini Andrew,
amesema hali ya siasa inavyokwenda, ni ngumu kwa vyama vya upinzani, kikiwamo
CUF kufanya vizuri katika wilaya ya Handeni.
Mwamini Andrew, aliyekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Kwamatuku mwaka 2010 kwa tiketi ya CUF.
Mwamini aliyasema hayo katika
mazungumzo marefu na Blog ya Handeni Kwetu kijijini Komsala, akielezea pia
mikakati yake kisiasa kwa ajili ya kuliletea maendeleo Taifa lake.
Mwanasiasa huyo chipukizi
alisema kuwa vyama vya upinzani vingi vinaelemea sana sehemu za mjini, huku
wakishindwa kubuni mipango ya kuwakomboa watu wa vijijini.
Alisema suala hilo
lilisababisha CUF lishindwe kutambua mchango wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2010 licha ya kuwa mgombea udiwani pekee katika wilaya ya Handeni aliyepata
kura nyingi, licha ya kuangushwa na diwani wa CCM.
“Hizi ni changamoto kubwa
ambazo huenda zikaangamiza siasa za Tanzania, maana vyama vingi vya upinzani
vinaona mjini ndio kila kitu, wakati wananchi wengi wapo vijijini.
“Jambo hili ndilo lililofanya
CUF washindwe kutambua umuhimu wangu pamoja na wengine wote, hivyo huenda
likazua kinyongo kwa uchapakazi wa sisi wawakilishi wao,” alisema.
Katika wilaya ya Handeni mkoani
Tanga, chama pekee kinachokubalika kwa wananchi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kikifuatiwa na CUF ambacho hata hivyo kinaonekana kupoteza thamani yake machoni
mwa wananchi wengi wilayani humo.
No comments:
Post a Comment