Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WIZARA ya Maliasili na Utalii, imewashukuru
watu wote waliotembelea wizara yao katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es
Salam na kuwawezesha kuibuka mshindi wa
Kwanza wa Banda Bora katika kundi la Taasisi za Serikali zilizoshiriki katika
maonyesho ya Kimataifa ya 37 ya Saba Saba 2013.
Ushindi mtamu ehe. Ndivyo wanavyofurahia wadau hawa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Ushindi huu unaama kubwa sana
kwetu kwani haikuwa rahisi kuhakikisha wananchi waliokuwa wakiingia kwa wengi
bandani kwetu wanapata elimu yakutosha kutoka kwa wataalamu na wadau mbalimbali
wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale waliokuwa wakitoa elimu
mbalimbali zikiwemo za uhifadhi endelevu wa wanyamapori, ufugaji nyuki na
utalii.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakijiachia katika maonyesho ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotumwa Handeni
Kwetu na Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Tulizo Kilaga, ilisema kuwa mwitikio huo
umewafanya wajione ni washindi katika maonyesho hayo ya kibiashara.
“Aidha wale ambao hawakujaaliwa
kwa sababu moja ama nyingine kufika kwenye banda letu wasiwe na wasiwasi wanaweza kuungana nasi
kwenye Maonyesho ya Nanenane Dodoma ambapo tutahakikisha tunafanya vema zaidi.
“Sambamba na hilo Wizara
inachukua fursa hii kuomba radhi kwa wale wote wailiokwaza kwa namna yoyote ile
katika kipindi chote cha Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara 37 kwani tunatambua
wananchi wengi mlikuwa na kiu ya kutembelea banda la wanyama hai hata muda
ambao tulilazimika kulifunga (saa kumi na mbili jioni) kutoa fursa kwa wanyama
kupumzika na kupata mlo wao wa usiku,” ilisema taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment