Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa jeshi la Polisi
wilayani Handeni, OCD Zuber Chembera, amewataka watu kuacha kuendesha pikipiki
kwa mwendo wa kasi, maana ni hatari kwa maisha yao.
OCD Zuber Chembera, aliyesimama.
Akizungumza juzi wilayani
Handeni, Chembera alisema kuwa kati ya wengi wanaopata matatizo barabarani hasa
waendeshaji wa pikipiki, ajali zao zimesababishwa na mwendo wa kasi.
Alisema pikipiki inapopata
ajali ikiwa kwenye mwendo wa kawaida, haiwezi kuleta madhara makubwa vikiwamo
vifo vinavyoendelea kutikisa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
“Ni bora tuambiane kuwa mwendo
wa kasi hauna maana, ukizingatia kuwa pikipiki zinaleta madhara kwa watu wengi
mno, hivyo tuache kukimbia bila mpango.
“Ajali nyingi za pikipiki
barabarani chanzo chake ni mwendo wa kasi, maana dreva wanaona ndio njia nzuri
ya kuwafikisha wanapokwenda, jambo ambalo si sahihi,” alisema.
Wilaya ya Handeni ni miongoni
mwa zile zinazokumbwa na ajali za pikipiki, wakati juzi katika kijiji cha
Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga, vijana wawili wamekufa baada ya
kugongana na baiskeli, huku mmoja akisalimika.
No comments:
Post a Comment