Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SIKU chache baada ya kuzindua albam yake 12, bendi ya Twanga Pepeta imepata pigo kutokana na mdau wake mkubwa,
ama ‘senator’ wake Mathew Kawogo maarufu kama ‘Mathew Kiongozi’ ametangaza
kuachia nafasi hiyo na kuwataka wadau wa muziki wa dansi Tanzania waheshimu
msimamo wake.
Mathew Kiongozi, aliyekuwa seneta wa Twanga Pepeta
Mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu
Bendi ya Twanga Pepeta, ilizundua albamu yake mwishoni mwa
wiki iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, iliyokwenda kwa jina
la Nyumbani ni Nyumbani.
Akizungumza mapema leo mchana, Mathew Kiongozi alisema
kuanzia leo yeye si seneta tena wa bendi ya Twanga Pepeta na kuamini kuwa
nafasi yake itazibwa na wadau wengine wa muziki wa dansi hapa nchini na
kuendeleza muziki wa dansi.
Alisema kuwa ameitumikia bendi hiyo kwa muda mrefu kwa
kujitolea kwa hali na mali, ila sasa umefika wakati wa kujiweka pembeni na
kuamini kuwa msimamo wako utakuwa mzuri kwake kwa ajili ya kujiweka huru zaidi.
“Nimekuwa karibu na Twanga Pepeta kwa muda mrefu mno sambamba
na kushiriki harakati nyingi za kimaendeleo juu ya bendi hii, ila sasa naona
nijiweke kando na kuwapisha wengine.
“Huu ni msimamo utakaoniweka huru na kuendelea kubaki shabiki
wa kawaida wa bendi hii na nyinginezo zote zinazofanya muziki wa dansi Tanzania
kwa ajili ya kukuza tasnia hiyo,” alisema Kiongozi.
Kutangaza kuachia nafasi yake, huenda ikawa pigo kwa bendi
hiyo inayoendeshwa na Mkurugenzi wake, Asha Baraka, huku ikifanikiwa kukaa
kileleni kwa kipindi kirefu tangu kuasisiwa kwake.
No comments:
Post a Comment