Na Kambi Mbwana, Handeni
WAANDISHI wa Habari hapa nchini
wameaswa kuandika habari kwa haki kwa kuelezea mabaya na mazuri ili jamii
iendelee kuishi kwa heshima ndani na nje ya nchi.
Salum Masokola, Katibu wa Mbunge Abdallah Kigoda, Handeni.
Hayo yalisemwa leo na Salum
Masokola, Katibu wa Mbunge wa Handeni, mkoani Tanga, Abdallah Kigoda, ambaye pia
ni Waziri wa Viwanda na Biashara.
Akizungumza na Handeni Kwetu
Blog ofisini kwake, Masokola alisema kuwa kuna baadhi ya waandishi wanachoweza
kufanya wao ni kuelezea mabaya tu na kuacha mazuri.
Alisema waandishi wa aina hiyo
ndio wale wanaosababisha mtafaruku kwa jamii hususan kwa viongozi wanaoandikwa
bila kuangalia mazuri yao waliyofanya kwenye jamii.
“Hali hii inasababisha baadhi
ya watu kuona kuwa serikali haijafanya mazuri wakati si kweli, hivyo kuna kila
sababu sasa ya waandishi kukaa kwenye haki.
“Wakifanya hivyo mambo yatakuwa
mazuri maana jamii itaishi kwa heshima na kuleta maendeleo yao kwa kushirikiana
na viongozi wao sehemu mbalimbali za Tanzania,” alisema Masokola.
Wilaya ya Handeni ni miongoni
mwa zile zinazopigania maendeleo ya wananchi wake, huku kwa sasa ikiwa chini ya
Mkuu wake wa wilaya, Muhingo Rweyemamu.
No comments:
Post a Comment