Naibu
Mkurugenzi Mtendaji, Mishack Ugulo, pichani.
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
WANAMICHEZO
mbalimbali wa mchezo wa gofu, jana walionyeshana uwezo katika mashindano
yaliyodhaminiwa na benki ya BankABC, yakihudhuriwa pia na viongozi wa juu ya benki
hiyo yenye matawi yake Dar es Salaam na Arusha.
Mashindano hayo
yalivutia wachezaji wengi, wakiwamo wafanyabiashara na wateja wa BankABC, huku
dhamira ikiwa ni kuendeleza juhudi za kuuweka mchezo wa gofu katika kiwango cha
juu.
Akizungumza katika
ufunguzi wa shindano hilo la siku moja katika Viwanja vya Gymkhana, yaliyoanza
asuhubi hadi jioni, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya BankABC, Misheck
Ugalo, alisema kuwa wameamua kudhamini shindano hilo ili kushiriki juhudi za
kuuletea mafanikio mchezo huo.
Alisema benki yao ina
haki ya kushiriki pamoja na wateja wao katika sekta ya michezo, ukiwamo gofu
unaopendwa na watu wengi.
“Leo (jana) tumeamua
kuwa na wateja wetu katika kudhamini gofu ambayo hakika ni mchezo mzuri
unaohitaji umakini katika uchezaji wake.
“Shindano hili la
siku moja nadhani litakuwa na tija hasa kama washiriki wote waliojiandikisha
kushindana wataonyesha uwezo wao halisi,” alisema.
Benki ya BankABC sio
mara yake ya kwanza kujiingiza kwenye michezo, hasa baada ya mwaka jana
kudhamini michuano ya ‘BankABC SUP8R 2012.
No comments:
Post a Comment