Wakili wa Lwakatare, Tundu
Lisu (kulia) akimuelekeza jambo Mbuge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati
wakijaribu kuandaa mipango ya dhamana.
Lwakatare
akionesha alama ya vidole viwili wakati akipelekwa
kizimbani.
Wanachama na mashabiki wa
Chadema wakionesha alama ya vidole viwili kabla ya kesi
kuanza.
Wakili Nyaronyo
Kicheere akimuelekeza jambo Godbless Lema baada ya kesi kuahirishwa, kulia ni
Tundu Lisu.
Wanachama wa Chadema wakiwa
wametawanyika nje ya mahakama baada ya kesi
kumalizika.
Mke wa Lwakatare
akitahayari baada ya mumewe kunyimwa dhamana.
Mkuu wa kitengo cha
usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilfred Lwakatare leo
amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es
Salaam na kusomewa mashitaka manne ya ugaidi.
Lwakatare amepandishwa
kizimbanai sambamba na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ludovick Joseph.
Katika kesi hiyo Lwakatare anatetewa na mawakili watano, Tundu Lisu, Profesa
Safari, Nyaronyo Kicheere, Mabere Marando na Peter Kibatara
No comments:
Post a Comment