Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, amekubali kuwaagiza watendaji wa Shirika la Posta Tanzania,
kuhakikisha kuwa wanatatua kero ya usambazaji wa kazi za wasanii pamoja na
kupatikana kwa stika za kukomesha wizi huo.
Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado
November, alipokuwa akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mashirikisho
mbalimbali ya wasanii, katika hali ya kutafuta namna ya kukabiriana na kero sugu
za wizi wa kazi za wasanii.
“Tunashukuru kuwa mambo yakienda sawa, Posta watahusika
katika usambazaji wa kazi za wasanii, ukizingatia kuwa wao wapo nchi nzima,
badala ya kuwaachia wafanyabiashara wachache.
“Kuna Watanzania wanataka kununua kazi za wasanii, lakini
wanakosa kazi hizo, hivyo kujikuta nao wakiingia katika wizi kwa kuchoma katika
vibanda vya wauzaji wasiokuwa na leseni za biashara hizo,” alisema.
Aidha, ujumbe kutoka Kampuni ya Africori inayohusika na
masuala ya uuzaji wa kazi za wasanii na usambazaji kwenye mitandao unatarajiwa
kuwasili kwa kufanya mazungumzo na wasanii mbalimbali ili kuingia nao
makubaliano ya kibiashara mapema mwezi
huu.
No comments:
Post a Comment