Kukipiga na Toto African kesho Jumamosi Mwanza
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Simba, umesema licha ya
kufungwa bao 1-0 dhidi ya timu ya Kagera Sugar, ila wachezaji wao wamecheza
soka la uhakika, ingawa nafasi ndogo zilizotumiwa na kocha wa Kagera, King
Abdallah Kibadeni, zilichangia kuwaua katika mchezo huo.
Juma Kaseja
Kibadeni ni kocha na mchezaji aliyewahi kuwika
na Simba kwa misimu kadhaa, kabla ya kuhamia pia kuinoa klabu hiyo ambayo kwa
sasa ipo chini ya Patrick Liewing na wasaidizi wake, Jamhuri Kihwelo Julio na
Moses Basena, raia wa Uganda, aliyewahi pia kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu wakiwa safarini
kutoka Bukoba kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kucheza na Toto African
Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga,
alisema nafasi ndogo walizopoteza na utaaamu wa Kibadeni vilichangia kuwaua na
kupata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Alisema pamoja na matokeo hayo, lakini kwa sasa
wanaelekeza nguvu zao dhidi ya Toto African, wakiamini kuwa watapata matokeo
mazuri na kuwafurahisha mashabiki wao katika mchezo huo.
“Kagera Sugar ipo chini ya Kibadeni, kocha
mwenye uzoefu na pia anawafahamu vyema wachezaji wote wa Simba kwa sababu
alikaa kwenye benchi kwa muda mrefu, hivyo kuna uwezekano alitumia ujanja huo
na kuchangia wao kuibuka na ushindi huo dhidi yetu.
“Hata hivyo, kwa sasa hatuangalii matokeo hayo
ya kufungwa, bali nguvu zote zipo mbele ya Toto African, ukizingatia kuwa
mchezo huu utapigwa keshokutwa (kesho) Jumamosi, katika Uwanja wa CCM Kirumba,
jijini Mwanza, “ alisema Kamwaga.
No comments:
Post a Comment