Shekhe Ponda, akiwa kwenye ulinzi mkali.
Washitakiwa 52 kati ya 54 katika kesi ya kula njama
na kufanya maandamano isivyo halali wamehukumiwa kwenda jela kila mmoja baada ya
kukutwa na makosa matatu huku mmoja akiachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia
na mwingine kufariki dunia kabla ya hukumu iliyotolewa leo na hakimu Sundi Fimbo
wa Mahakama ya Hamimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Baada ya pande zote kusikilizwa na washtakiwa kutoa
hoja za utetezi, hatimaye hakimu Fimbo alitoa hukumu hiyo leo ambapo aliwatia
hatiani washtakiwa 52 kwa makosa matatu kati ya manne na kila mmoja akamhukumu
kwenda jela mwaka mmoja kwa kila kosa.
Hata hivyo, Fimbo akasema washtakiwa hao watakwenda
kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa vile adhabu zote zinakwenda kwa
pamoja.
Mshitakiwa aliyeachiwa huru baada ya kukutwa kuwa
hana hatia ni Waziri Omari (namba 48), ambaye katika utetezi wake alidai kwamba
siku ya tukio alikamatwa wakati akiwa katika shughuli zake za biashara ya kuuza
kwa kutembeza barabarani vyombo vya nyumbani ikiwa ni pamoja na
mabeseni.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo leo, wakili
Mohamed Tibanyendera alimtaka hakimu awapunguzie adhabu wateja wake kwavile
wengi wao wanategemewa na familia zao na kwamba, tayari walishakaa mahabusu kwa
kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.
Washitakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Salum
Makame, Said Idd na Ally Nandumbi, Makame, Idd na Nandumbi, Hussein Athumani,
Seif Rwambo, Abdull Ally, Waziri Swed, Naziru Waziri, Ahmad Rashid, Jumanne
Kayogola, Hamis Tita, Amri Diyaga, Salum Said, Rajabu Mpita na Haji Sheluhenda,
Abdul Ahmed, Bakari Mwambele, Ramadhani Fadhili, Awadh Juma, Omari Mkwau, Kassim
Chobo, Abubakari Bakari, Ramadhani Milambo, Hamis Ndeka, Athuman Juma, Abdallah
Salum, Juma Makoti, Bashir Kakatu, Imam Omari, Rashid Lukuta na Bakari Athumani,
Mbwana Kassim, Nurdin Ahmed, Mustapha Mide, Rajabu Kifumbo, Zuberi Juma, Omari
Mkandi, Idrisa Katulimo, Sawali Mola, Said Dudu, Ramadhani Juma, Musa Sinde,
Issa Sobo, Yahaya Salum, Jabil Twahil, Shomari Tarimo, Hashim Bendera, Waziri
Toy, Athuman Yahaya, Yasin Seleman, Shaban Malenda, Yasin Mohamed, Khatib
Abdallah na Rajabu Rashid wote wakazi wa jijini Dar es
Salaam.
Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya tukio, wilaya ya
Ilala, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama za
kufanya maandamano isivyo halali.
Shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio
la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kusababisha
uvunjifu wa amani.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola,
alidai katika shitaka la tatu kuwa siku na eneo la tukio la kwanza na la pili,
washtakiwa wote kwa pamoja baada ya Jeshi la Polisi kutoa zuio la kufanya
maandamano, walikiuka amri hiyo na kufanya mkusanyiko ulisababisha vurugu na
uvunjifu wa amani.
Katika shitaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa
Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi
vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, vilio vilitawala
katika viunga vya mahakama vilivyofurika watu kufuatia baadhi ya ndugu na jamaa
wa washtakiwa kuangua kilio, wasiamini kile
kinachotokea.
Baadaye washtakiwa walipandishwa kwenye karandinga
na kupelekwa
gerezani.
No comments:
Post a Comment