Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kagasheki,
akizindua rasmi kikundi cha Habari Group kinachojumuisha waandishi kutoka
vyombo mbalimbali vya Habari, ufunguzi uliofanyika Hoteli ya Lamada, jijini Dar
es Salaam juzi. Anayeshuhudia kushoto ni Mratibu wa kikundi hicho, Rabia Bakari
na wageni wengine waalikwa. Picha na Kambi Mbwana.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kagasheki,
amewataka wanawake kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wao, ikiwa ni
pamoja na kuendelea kujiunga kwenye vikundi.
Kagasheki aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika ufunguzi
wa kikundi cha waandishi wa habari wanawake kutoka vyombo mbalimbali vya
habari, kinachojulikana kama Habari Group.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Kagasheki alisema ili
uchumi wa Tanzania kukua, ni pamoja na kuona wanawake wanajiwezesha zaidi kwa
kufanya biashara mbalimbali kwa kupitia vikundi vyenye uwezo mkubwa wa
kusaidiwa pamoja na kukopeshwa.
Alisema mara baada ya kualikwa kwenye uzinduzi wa kikundi
cha Habari Group kinachojumuisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya
Habari, alijisikia faraja akiwa akiwa na lengo la kuwawezesha ili maisha yao
yawe mazuri kwa mjumuiko huo.
"Naunga mkono juhudi zenu za kila aina katika
kuhakikisha kuwa mnajikomboa kuanzia mwanzo wa ufunguzi huu na kuendelea, maana
nyie waaandishi habari mkijikwamua, naamini Uchumi unaotakiwa utafika mahali
pazuri.
"Naomba muendelee kuwa pamoja na kubuni vitu vyenye
tija katika maisha yenu, maana ili muendelee, ni wazi vikundi vya aina hii
vinatakiwa kuendelea kuundwa kwa kila sekta," alisema Kagasheki.
Awali mratibu wa kikundi hicho cha Habari Group, Rabia
Bakari, aliwashukuru wahudhuriaji wote katika hafla ya ufunguzi huo, Angela
Kairuki, ambaye ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, pamoja na wadau mbalimbali
wa maendeleo, ikiwamo PPF na wengineo.
mwisho
No comments:
Post a Comment