Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Taifa Stars imeanza
kambi jana jioni (Machi 16 mwaka huu) ambapo wachezaji 14 kati ya 23 walioitwa
wameripoti na kufanya mazoezi leo asubuhi chini ya Kocha Kim Poulsen.
Wachezaji walioripoti ni
nahodha Juma Kaseja kutoka Simba na msaidizi wake Aggrey Morris wa Azam, Erasto
Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud
Cholo (Simba), Shomari Kapombe (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Wengine ni Athuman Idd
(Yanga), Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba),
Mrisho Ngasa (Simba) na Simon Msuva (Yanga).
Wachezaji Hussein
Shariff, Issa Rashid na Shabani Nditi ambao timu yao ya Mtibwa Sugar jana
ilicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) mjini Turiani wataripoti kambini
leo jioni.
Kikosi hicho
kitakamilika Jumanne asubuhi baada ya wachezaji walio katika kikosi cha Azam
nchini Liberia kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho kurejea nchini. Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemorasi ya
Congo (DRC) wanatarajiwa kutua nchini kesho usiku.
No comments:
Post a Comment