Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KADA na Mchumi wa CCM
Kata ya Makumbusho, Yusuph Shaban Mhandeni, maarufu kama Yusuphed Mhandeni,
jana aligawa kadi za uanachama wa klabu ya Yanga, kwa tawi la Green Stone,
Mwananyamala, ikiwa ni baada ya kutolewa Makao Makuu ya klabu ya Yanga.
Makabidhiano hayo
ambayo yalifanyika kwenye tawi lao, yaligubikwa na shangwe, huku miongoni mwa
waliopewa kadi hizo, akiwa ni nguli wa muziki wa taarabu nchini, Malkia Khadija
Omari Kopa.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam kwenye makabidhiano hayo, Yusuphed Mhandeni, alisema kuwa
atafanya kila analoweza kuhakikisha kuwa tawi hilo linakuwa kubwa ili wanachama
hao waweze kushirikiana kwa karibu na uongozi w Yanga uliopo madarakani kwa
maendeleo ya klabu yao.
Alisema awali
alifurahia kusikia kuanzishwa kwa tawi hilo, hivyo lengo lake ni kuwaunganisha
wananchi wakiwamo wapenzi na wanachama wa Yanga na kufahamu njia nzuri za
kuiwezesha Yanga.
Yusuph Shaban Mhandeni,
Yusuphed Mhandeni, akimpa kadi yake mwanachama wa Yanga, Tawi la Green Stone,
anayejulikana kwa jina la Abdul Sengwila, jijini Dar es Salaam jana. Endelea kuisoma habari hii hapo chini.Waliokabidhiwa kadi wakizionyesha kwa na furaha tele.
Yusuphed Mhandeni wa tatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma, akiwa na wanachama
wa Yanga kwa kupitia tawi la Green Stone, Mwananyamala, huku wakiongozwa na
mwenyekiti wao wa tawi hilo, Lumolwe Matovolwa, maarufu kama Big ambaye pia ni
msanii maarufu wa filamu hapa nchini.
"Nashangaa watu
wenye mapenzi mema na michezo wapo wengi, lakini wapo kimya, hivyo naapa
kushirikiana na nyinyi kwa kila hatua, ikiwapo kuwalipia kuwanunulia kadi watu
ambao hawatakuwa na uwezo huo, hasa wazee watano tutakaowathibitisha ili tuwe
nao.
"Mbali na
kuwalipia kadi hizo, pia nitashirikiana na viongozi waliopo hapa kwa kila
jambo, ikiwapo pia kugharamia safari moja ya mkoani kabla ya ligi kumalizika
kama wanavyofanya wengine kwa ajili ya Yanga,” alisema Mhandeni.
Green Stone
lilianzishwa rasmi mapema mwaka huu likiwa chini ya viongozi wa muda,
Mwenyekiti ni Lumolwe Matovolwa maarufu kama ‘Big’ na Katibu wake ni Ally
Regani, ambao kwa mara ya kwanza wamepewa kadi tano Makao Makuu ya Yanga kwa
ajili ya kuwapa wanachama wao.
Watu ambao
wamekabidhiwa kadi hizo na Mhandeni ambaye ni kama mlezi wa tawi hilo ni pamoja
na Filbert Mbezi Simon, Abdu Sengwila, Rajabu Mbwana, Joseph Joseph Chilumba,
Anthon Amulike na Khadija Kopa ambaye yeye hakuwapo kwenye makabidhiano hayo.
No comments:
Post a Comment