Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama Cha Soka
wilayani Korogwe, Peter Juma, amesema licha ya kuwa na changamoto za hapa na
pale, lakini ligi yao iliyoanzishwa na Mkuu wa Wikaya, Mrisho Gambo inaendelea
vizuri kwa vijana kuonyesha vipaji vyao.
Mrisho Gambo, Mkuu wa wilaya Korogwe
Akizungumza kwa njia ya
simu, Juma alisema kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa
katika ligi hiyo, ikiwamo uwezo wa uchezaji wa vijana wao.
Alisema ligi hiyo yenye vituo
nane wilayani humo, pia ina ushindani wa aina yake, hivyo wanaamini kuwa lengo
haswa la kuwaweka vijana pamoja na kujadili suala la michezo limefanikiwa.
“Namshukuru DC kwa kuanzisha
ligi ya Gambo Cup wilayani Korogwe, maana tunajua kuwa ni njia nzuri ya
kutupatia mafanikio katika suala zima la mpira wa miguu.
“Timu nyingi zimejitokeza na
zinashiriki kwa kasi ya ajabu, hivyo tunaamini kuwa ni njia moja wapo ya
kutangaza vipaji vya wachezaji wetu kwa kupitia mashindano ya Gambo Cup,”
alisema.
Vituo ambavyo vinashiriki mashindano
hayo ya Gambo Cup wilayani Korogwe ni pamoja na Bungu, Kelenge, Old Korogwe,
Kwamndolwa, Kwamsisi, Makuyuni, Mswaha, Mombo na New Korogwe, iliyopo Korogwe mjini.
No comments:
Post a Comment