Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HALI ya uokoaji katika jengo la
ghorofa 16 lililoanguka jana mtaa wa Indira ghandi, Kariakoo jijini Dar es
Salaam inaendelea, huku hadi sasa watu 18 wakiwa wamekutwa wameshapoteza
maisha.
Pichani, uokoaji ikiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Said Meck Saidik, alitembelea muda sio mrefu kwa ajili ya kujionea hali ya
uokoaji inavyoendelea katika eneo hilo lililoibua taharuki kubwa.
Jana, Rais wa Tanzania, Jakaya
Mrisho Kikwete, alitembelea pia katika eneo hilo na kujionea jinsi
lilivyoanguka na kusababisha mtafaruku mkubwa kwa watu waliokuwa kwenye kadhia
hiyo.
Juhudi za kuokoa watu waliokuwa
kwenye ajali hiyo zilipamba moto dakika chache baada ya habari hizo kufika kwa
vyombo vya Dola, huku viongozi wa vyama vya siasa na serikali kuwa bega kwa
bega katika kufanikisha juhudi za kunusuru roho za watu wao.
Mwili mmoja umeopolewa muda
mfupi uliopita, ikiwa ni masaa kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,
Sadik kufika, wakati tayari idadi ya watu 17 ilishatangazwa tangu jana.
No comments:
Post a Comment