Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HELEN Joseph, bondia mwanadada ambaye anaishi katika jiji la Accra, nchini Ghana akipigana ngumi yuko mbioni kupanda kilele cha mafanikio katika maisha yake ya ngumi.
Ni wakati ambao Helen Joseph
anayetoka katika nchi ya Nigeria aliokuwa anaungojea katika maisha yake ya
ngumi.
Mwaka
jana alikutana na bondia Dahianna Santana katika jiji la San Domingo, nchini
Dominican Republic kugombea ubingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa Unyonya
(Fearherweight).
Taabu na kashikashi zote alizozipata wakati wa patashika ile
ya mwaka jana zimekuwa fundisho tosha kwa Helen wakati anapojiandaa kukutana na
Marianna Gulyas kutoka nchini Hungary kugombea ubingwa wa IBF wa mabara katika
uzito wa unyoya.
Mpambano
huo, unaoandaliwa na kampuni maarufu ya kukuza ngumi ya GoldenMike Boxing
Promotion Syndicate ya nchini Ghana unategemea kuwa wa patashika kweli kutokana
na mabondia wote wawili kuwa na ujuzi tele ulingoni. Wawili hawa watakutana
tareeh 30 March katika uwanja wa michezo wa Accra na mpambanohuu utarushwa moja
kwa moja na luninga ya Super Sports.
Ni
mapromota wachache na mameneja wachache ambao wanaweza kuwekeza kiasi
kikubwa hivyo cha pesa katika mchezo wa ngumi namna ambapo kampuni ya
GoldenMike Boxing Promotions Syndicate ya nchini Ghana imewekeza katika kuinua
kipaji cha mwana dada Helen Joseph.
Kwa
upande wake Helen ambaye ni nadhifu, mtanashati na mwenye nidhamu ya hali ya
juu, mchezo wa ngumi ndio unaomlisha katika maisha yake na atatumia uwezo wake
wote kuhakikisha kuwa taji hli kubwa la ngumi linabaki barani Afrika na
kulitumia kama ngazi ya kukutana tena na Dahianna Santana katika ubingwa wa
dunia!
No comments:
Post a Comment