Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
MCHEKESHAJI maarufu na mwimbaji
wa muziki wa Injili nchini, Emmanuel Mgaya, Masanja Mkandamizaji, amesema kuwa
amejipanga imara kuhakikisha kuwa anafanya vitu vya aina yake katika onyesho la
Tumaini Jipya, linalotarajiwa kufanyika mkoani Morogoro Machi 31, katika Uwanja
wa Jamhuri na kushirikisha pia wakali mbalimbali.
Masanja Mkandamizaji
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Masanja alisema kuwa amejiandaa vyema kutangaza neon la Mungu kwa
kupitia kipaji chake cha uimbaji wa muziki wa Injili, akiamini kuwa afya yake
itakuwa njema na kuimba pamoja na wadau wao katika onyesho hilo la Tumaini
Jipya.
Masanja Mkandamizaji
Alisema ingawa anatamba sana
katika ulingo wa uchekeshaji kwa kuwa na aina ya uzungumzaji na kufurahisha
watu wengi, lakini makali yake hayaelezeki katika uimbaji wa muziki wa injili.
“Nipo sawa kiafya na naamini
Mungu atanibariki kila zuri kwa ajili ya kuimba pamoja kwenye tamasha hilo la
Tumaini Jipya nikiwa na waimbaji wengine wenye makali ya aina yake.
“Itakuwa ni siku nzuri kwa siku
ya Jumapili ya Machi 31 katika uwanja huo wa Jamhuri, hivyo naamini watu
watakuja kwa wingi kulishuhudia neno likipenya masikioni mwao,” alisema Masanja
Mkandamizaji.
Mbali na Masanja, wengine
watakaofanya onyesho hilo ni pamoja na Martha Mwaipaja, Stara Thomas, Bahati
Bukuku, Sifa John, Joseph Nyuki pamoja na vikundi mbalimbali vya kwaya
vikitajwa kuwapo kwenye tamasha hilo la Tumaini Jipya litakaloanzia mkoani
Morogoro.
No comments:
Post a Comment