Mwani
Nyangassa, akiandaa keki hii ambayo hakika imeniweka kwenye shangwe kupita
kiasi. Hii ni siku yangu muhimu mno. Zaidi, inanifanya niamini kuwa bado
tunapaswa kuishi kwa amani na upendo, ukizingatia kuwa sijatoa hata mia yangu.
Huu ni upendo wa aina yake kutoka kwa Mwani Nyangassa na wafanyakazi wote wa
New Habari 2006 Ltd.
NIKABAKI kimya. Sikuwa na neno la kusema, zaidi ya kutumbua
macho yangu, kama vile natafuta panya aliyechukua pochi yangu yenye mia tano ya
kunifikisha kwenye msiba wa ndugu au mtu mwingine wa karibu na mimi.
Ndivyo ninavyoweza kuielezea siku hii, tukio la kushtukizwa
la kupewa keki katika kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa, ninayoadhimisha kila
Machi 14. Nakumbuka, niliinuka kwenye kiti change, nikitoka nje, ambapo ghafla
nikasikia wimbo huu, Happy Birthday Kambi.
Sauti thabiti kutoka kwa akina dada hawa wawili, Mwani
Nyangassa, ambaye licha ya kuwa ni dada yangu wa karibu mno, ila kikazi pia ni
bosi wangu, akiwa sambamba na mwanadada Jenifer Ullembo, wote tukiwa kwenye
Kampuni ya New Habari 2006 Ltd.
Pamoja na kudanganywa kikao na bosi wangu Mwani Ngangassa,
lakini pia najiuliza gharama za keki hii imetoka kwa ajili ya Kambi Mbwana.
Hakika, natumia muda mwingi kufikiria namna gani ya kuwalipa watu hawa kwa moyo
wao wa upendo.
Nashukuru, zaidi nikihakikisha kuwa kuwa katika kipindi cha
uhai wangu, kuna mengi ambayo aidha kwa wakati mwingine hayakuwa mazuri, lakini
wafanyakazi hawa waliniunga mkono na kunifariji. Hakika haya ni matukio makubwa
mno.
Huwatokea watu mara chache mno kwa mwaka, maana tukio la leo
ni kati ya yale ambayo nitakabi nayawaza katika kipindi change cha maisha ya
duniani. Nakumbuka kauli ya dada Mwani Nyangassa, akiitoa kama bosi, Mhariri wa
Michezo wa Gazeti la Mtanzania.
"Kambi usiende popote tuna kikao leo kujadili utendaji
wetu wa kazi,” ilikuwa kauli ya kuelezea kuwa kumbe muda ujao tungekaa na
kujadili kazi zetu. Sawa, lakini huyu naye aliniambia, anaitwa Mohamed Mharizo
kuwa, umeambiwa kuhusu kikao, basi usiende popote Mkurugenzi wa Handeni Kwetu,”
alisema Mharizo.
Sikujua lolote zaidi ya kusema asante, sitakwenda popote
zaidi ya kusubiria kikao hicho baada ya muda wake kufikia. Haya ndio maisha.
Haya ndio matokeo ya kuishi kwa upendo na watu wote bila kuangalia ni mtu wa
aina gani.
Natumia fursa hii kuwaombea kwa Mungu kwa kila aliyeshiriki
kwa namna moja ama nyingine katika kusherehekea siku hii adhimu. Bosi wangu,
Kulwa Karedia, Novacatus Makaranga, Bakari Kimwanga, Grace Hoka, Denis
Luambano, Simon Regis, Hassan Bumbuli, Anthon Siame, Jonathan TiTO, Selemani Shineni,
Asham Haji, Evance Magege na wafanyakazi wote wa New Habari, bila kusahau
kumuombea Mungu Mhariri Mtendaji wetu, Absalom Kibanda, nikiamini kuwa Mungu
ataendelea kumpigania na kurudisha afya yake ili arejee kwenye majukumu yake ya
Kitaifa.
Hakika, hili ni tukio kubwa kuwahi kunitokea katika maisha
yangu na naomba Mungu awe upande wangu kwa kunipa hekima, busara, utulivu na
unyenyekevu, sambamba na kuwaombea amani Watanzania wote.
Asante dada Grace Hoka kwa upendo wako kwangu.
Asante Jennifer Ullembo kwa ushirikiano wako na moyo wako.
Mhariri wa Mtanzania, Kulwa Karedia
Hivi ndivyo ilivyokuwa hii keki
Denis Luambano, akijiandaa kula keki
Shoo naye alikuwapo jamani
Hapo sasa. Hapo najiandaa kula keki hii kutoka kwa Mohamed Mharizo
Hizi ni baadhi ya picha nyingi zilizopigwa na Mpiga Picha
wetu, Zuberi Mussa, akiwa ni miongoni mwa watu muhimu walioifanya siku yangu
hii kuwa ya aina yake. Asanteni sana.
No comments:
Post a Comment