Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Iddy Mkwela wa Dar es salaam anatarajia kuoneshana
kazi ya kurushiana makonde na Lucas Ndula wa Muheza wakati wa kusherekea Sikukuu za Pasaka Jumapili ya Machi 31 katika viwanja vya wazi vya Jitegemee
vilivyopo wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa mpambano
huo wa raundi 6 kg,60 bondia wa siku nyingi ambae kwa sasa ni kocha wa mchezo
huo Muheza, Chalres Muhilu ' Spins' alisema mpambano huo wa wazi umeandaliwa
kwa ajili ya kutoa burudani wilayani hapo na kuhamasisha mchezo wa masumbwi
Ambapo kutakuwa na mapambano mengi ya mchezo huo
yatakayoanza saa kumi jioni ikiwa kiingilio ni miguu yako tu amewataka wapenzi
wa mchezo huo kujitokeza kuangalia mabondia kutoka Dar wakipambana na Muheza
pamoja na kutoa rai kujitokeza kwa wafadhili kudhamini mchezo huo unaopendwa na
vijana wengi wilayani humo ndio mana tumeamua kuweka katika viwanja vya wazi
ili watu wote wajionee wenyewe mchezo wa ngumi unavyo endeshwa katika mazingira
magumu
Nae Kocha wa kimataifa wa mchezo huo Rajabu Mhamila
'Super D' aliyepewa jukumu la kwenda na vijana kutoka Dar ili wakalete
changamoto na kuleta amasa ya mchezo huo amesema atakwenda na Nassoro Mbwiga
atakayemenyana na Bakari Sendekwa katika uzito wa kilo 52 na Iddy Mkwela atakaepambana
na Lucas Ndula mpambano wa raundi 6
Mbali
na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya
mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones, Miguel
Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo.
Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia
mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia
kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika
Mpambano ili kuweza kujifunza mambo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
No comments:
Post a Comment