Waziri
mkuu Mizengo Pinda (mwenye miwani) akisaidiwa kutundika mzinga wa kisasa na
naibu waziri wa mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu (kushoto) na mkuu wa
mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone, kwenye maadhimisho ya utundikaji
mizinga kitaifa uliofanyika katika kijiji cha Aghondo Manyoni Magharibi.
Waziri
mkuu Mizengo Pinda, akihutubia kwenye kilele cha utundikaji mizinga kitaifa
uliofanyika katika kijiji cha Aghondi jimbo la Manyoni magharibi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dk.Mary Nagu, akitoa nasaha zake kwenye kilele
cha utundikaji mizinga kitaifa uliofanyika katika kijiji cha Aghondi jimbo la
Manyoni magharibi.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amewaagiza watendaji na viongozi mbalimbali,
kuhamasisha vijana kujiunga/kuanzisha vikundi vya ufugaji nyuki ili waweze
kupambana vema na umaskini pamoja na uhaba wa ajira.
Mh. Pinda ametoa agizo hilo wakati
akizungumza kwenye kilele cha siku ya utundikaji mizinga kitaifa uliofanyika
katika kijiji cha Aghondi jimbo la Manyoni Magharibi.
Amesema kazi ya ufugaji wa nyuki
ni rahisi mno na ni tofauti na shughuli zingine za kiuchumi ikiwemo ya kilimo
na ufugaji.
Waziri Mkuu amesema pamoja na
urahisi huo, lakini ndiyo kazi nzuri ambayo ina uwezo mkubwa wa kumkomboa
mhusika kiuchumi, kwa madai kwamba mazao ya ufugaji nyuki, yana soko zuri la
uhakika wakati wote.
Mh. Pinda amesema kwa hali hiyo,
upo umuhimu mkubwa kwa watendaji na viongozi kuhamasisha vijana kwa
bidii, ili waweze kujiunga katika vikundi na kwa njia hiyo watakuwa
wamejijengea mazingira mazuri ya kuweza kupewa misaada mbalimbali ikiwemo ya
kuwawezesha kufuga nyuki.
Katika hatua nyingine Waziri mkuu
almesema ufugaji wa nyuki utasaidia sana kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
Amesema kutokana na ukweli huo
mazingira yakitunzwa vizuri na kulindwa pamoja na mambo mengine, nchi itarudi
kwenye neema ya mvua zenye kheri.
No comments:
Post a Comment