Rais Jakaya Kikwete akikata
utepe kuashiria ufunguzi wa Uwanja wa Azam uliopo Mbande, Temeke Dar es Salaam
jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Bakharessa,
Abubakar Bakharessa na wa kwanza kushoto
ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Dk. Fenella Mukangara na wa
kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Mecky Sadick.
|
Rais akipokea zawadi ya jezi toka kwa Abubakar Bhakherssa ambaye ni mkurugenzi wa wakurugenzi wa kampuni ya Bakharessa |
Rais akisogeza kitambaa kuashiria uzinduzi
|
Hapa anatembezwa kwenye uwanja wa nyasi bandia |
Hapa anatembezwa uwanja wa nyasi asilia |
Rais akisalimia na wachezaji wa Azam A kabla ya kuanza mchezo ndidi ya Azam B |
Makocha wa Timu za Taifa na viongozi mbalimbali wa TFF walikuwepo |
Hapa yupo kwenye swimming pool |
Burudani pia ilikuwa sehemu ya sherehe |
"Lazima mtuchangie vijana wenu" Wacheza ngoma wakitembeza bakuli baada ya kucheza bila kuona mtu aliyekuja kuwatunza. |
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dr.Jakaya Kikwete leo
amezindua rasmi uwanja wa Azam na kuziponda Simba na Yanga kwa kushindwa
kumiliki viwanja vyao wenyewe badala yake wameendeleza migogoro
Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Dar es Salaam alipata
wasaa wa kuzungumza na maelfu ya wakazi wa jiji hili baada ya kujionea
kazi nzuri inayofanywa na Azam na kuipongeza kwa kufanikiwa kusonga
mbele kwenye mashindano ya shirikisho.
"Naipongeza Azam kwa kuwekeza kwenye ufundi na siyo kamati za ufundi
kama zinavyofanya vilabu vyetu vikubwa kwa maana kama ingekuwa kamati za
ufundi zinasaidia bara la afarika tungekuwa tunachukuwa kombe la dunia
kila linapofanyika" alisema Rais
Wakati akiyasema hayo maelfu ya watu walikuwa wakimshangilia kwa kuonyesha kuwa nachokisema ni kweli.
No comments:
Post a Comment