Sehemu ya shule ya mafunzo ya dini
iliyofungwa
Rais wa senegal Macky Sall, anasema kuwa serikali itafunga shule zote za mafunzo ya dini ambazo zitakosa kutimiza mahitaji ya usalama kwa watoto.
Matamshi yake Rais Macky Sall,
yanajiri baada ya watoto tisa kufariki katika ajali ya moto katika shule iliyo
karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Dakar.
Moto huo, ulizuka wakati watoto 45
wa shule wenye kati ya umri wa miaka sita na kumi na mbili, wakiwa ndani ya
chumba kimoja katika eneo la Medina.
Inaarifiwa huenda mshumaa ndio
ulisababisha ajali hiyo ya moto uliozuka Jumapili jioni.
Baada ya kuzuru eneo la ajali, bwana
Sall, alisema kuwa shule za mafunzo ya kidini ambazo zinawadhulumu watoto na
kukosa kuhakikisha usalama wao, lazima zifungwe.
''Watoto watarejeshwa kwa familia
zao,'' aliongeza rais Sall
Mwandishi wa BBC Thomas Fessy mjini
Dakar, alisema kuwa makundi ya kutetea haki za binadamu, yalionya dhidi ya
mazingira mabovu ambamo watoto wanaishi kama makaazi yao kwenye shule za
mafunzo ya dini na baadhi ya walimu wanawadhulumu watoto.
Wanafunzi wengi wanajulikana kama
"talibes" kwa lugha ya kiasili, na husihia kuomba omba chakula na
pesa mitaani na kisha kuwapelekea walimu hao.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment