Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini.
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
MABINGWA wa zamani wa
Tanzania Bara, Yanga SC, leo inaingia uwanjani kumenyana na timu ya Toto
African ya jijini Mwanza, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam.
Mbali na Yanga na Toto
African, mechi nyingine itakayochezwa leo itahusisha timu ya Polisi Morogoro
dhidi ya Azam, itakayochezwa katika Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo kati
ya Yanga na Toto, mwamuzi atakuwa ni
Andrew Shamba kutoka
Pwani, akisaidiwa na Abdallah Mkomwa pamoja na Abdallah Rashid wote kutoka
mkoani Pwani, wakati Kamishna ni Salim Singano kutoka Tanga, wakati Mtathmini
wa waamuzi amepangwa kuwa Alfred Lwiza.
Kocha wa timu ya Yanga,
Ernest Brandit, ametangaza hali ya hatari kwa timu ya Toto African, akisema
kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa wanatoka na pointi tatu na kutwaa
ubingwa wa Bara.
Yanga inaingia uwanjani
huku wakiwa na pointi 42, akifuatiwa na Azam yenye pointi 36, timu ambayo nayo
ipo kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutwaa ubingwa huo.
Nayo Azam ikiwa chini ya
kocha wao Stewart Hall, yenyewe imepania vilivyo kuhakikisha kuwa wanaibuka na
ushindi kwa ajili ya kujipatia pointi 29, wakiamini kuwa watazidi kusumbuana na
vinara wa ligi hiyo, ingawa Hall hatakuwa kwenye benchi la timu yake kwasababu
ya kufungiwa mechi tatu na Kamati ya Ligi kwa kitendo chake cha utovu wa
nidhamu.
Mwamuzi wa mchezo wa
Azam na Polisi amepangwa kuwa Charles Komba kutoka mkoani Dodoma, wakati Simon
Mberwa kutoka mkoani Pwani, atakuwa Kamishina.
No comments:
Post a Comment