Meneja
Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati akitangaza kwamba
Airtel kufanya Matamasha ya Airtel Yatosha katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania yenye lengo lan kutoa burudani sambamba na kuelimisha Jamii na
wateja wake kuhusu huduma za Airtel ikiwemo kuitambulisha huduma mpya
ya Airtel Yatosha. Kulia Meneja Mauzo Airtel Kanda ya Pwani Raphael
Daudi
Kiongozi
wa Tip Top connection Bwana Madee ni moja ya kikundi kitakachotumbuiza
katika Matamasha ya Airtel Yatosha akiongea wakati wa uzinduzi wa
Matamasha hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel morocco, Matamasha
haya yatawashirikisha wasanii wengine wakiwemo Fid Q, Juma Nature,
Ney wa Mitego na Stamina.Kulia Meneja Mauzo Airtel Kanda ya Pwani
Raphael Daudi
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Airtel
Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kufanya matamasha ya Airtel
Yatosha yenye lengo la kutoa burudani na kuwaelimisha jamii na wateja
wake juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel ikiwemo huduma
mpya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao
wowote kwa gharama nafuu zaidi.
Akiongea
wakati wa kutambulisha matamasha hayo, meneja uhusiano wa Airtel Bwana
Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kutoa burudani wakati wa msimu
huu wa sikukuu ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma yetu ya Airtel
yatosha kwa watanzania, tunaamini kwa kupitia matamasha yatakayofanyika
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania wateja wetu na watanzania kwa
ujumla watapata burudani na kupata nafasi ya kupata elimu juu ya huduma
zetu Nyingi
“Safari
yetu ya burudani za Airtel yatosha itaanza katika Mkoa wa Morogoro
katika siku ya Jumapili na Jumatatu ya Tarehe 31/3 na 01/04/2013,
Kuanzia Saa Tatu kamili Asubuhi mpaka saa Kumi na Mbili Jioni, pale
katika viwanja vya Sabasaba.
Tutakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Fid Q, Juma Nature, Ney wa Mitego na Tip Top Connection. Kiingilio ni BURE ,
tunapenda kukukualika wewe na washikaji zako wote kuhudhuria katika
tamasha hili la kwanza kabisa pale morogoro na utape burudani kabambe.
Njoo na Kitambulisho chako ili uunganishwe na ufurahie ofa nyingi toka
Airtel” aliongeza Mmbando
Naye
kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee alisema” kama kawaida
tumejipanga kuwapa wateja wa Airtel na watanzania burudani ya Ukweli
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, tunaomba watanzania wajitokeze kwa
wingi katika matamasha haya ya Airtel Yatosha. Mbali na sisi kutoa
burudani itakuwa nafasi pia kwetu kuona vipaji mbalimbali vya mashabiki
wetu ambao ndio wasanii nyota wa kesho hivyo tuwapa hamasa ya kujitokeza
kwa wingi ili tuweze kuburudika pamoja.
Wasanii
watakaoshiriki katika Matamasha maalumu ya Airtel yatosha watatumbuiza
kwa vibao vyao mahiri kama vile Fid Q na kibao chake cha Sihitaji
Marafiki na Ney wa Mitego na kibao chake cha Nasema Nao huku Tip Top
Connection wakiwakilisha na kibao chao cha Nani kamwaga pombe yangu
Airtel
hivi karibuni imezindua huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha
mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa
gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha
kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.
Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99#
No comments:
Post a Comment