Nadine, mnenguaji wa Extra Bongo na repa wake Papy Catalogue
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Extra
Bongo, leo inafanya shoo ya nguvu katika viwanja vya Garden Breeze, Magomeni,
katika bonanza lao la kila Jumapili linalohudhuriwa na mashabiki lukuki
wanaokwenda kupata burudani katika sehemu hiyo inayopendwa na wengi kwa sasa.
Extra Bongo,
maarufu kama Wazee wa Kizigo ama Next Level, inapanda jukwaani ikiongozwa na
Mkurugenzi wake, Ally Choki, akishirikiana na wakali kadhaa katika tasnia ya
muziki wa dansi hapa nchini, akiwamo Ramadhan Masanja, Banza Stone.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Choki alisema kuwa bonanza lao linapendwa na wengi, jambo
linalowasukuma mashabiki wao waende kwa wingi kujipatia burudani za aina yake
katika kuhakikisha kuwa wote wanapata burudani za aina yake.
Alisema kila
Jumapili, bendi yao inafanya shoo katika viwanja hivyo vya Garden Breeze, huku
ikihudhuriwa na watu wengi kutoka shemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam
wanaokwenda kupata ladha za Wazee wa Kizigo.
“Extra Bongo ni
bendi ya kazi sio ya kupiga porojo, hivyo naomba wadau waendelee kuja kwa wingi
katika shoo zetu, ikiwapo ya bonanza la Garden Breeze, ukizingatia kuwa
limeandaliwa maalumu ya kwa ajili ya kukutanisha watu wote.
“Kila mmoja
anaweza kuingia, maana halina gharama, ukizingatia kuwa tangu tuanze bonanza
letu tumekuwa na malengo madhubuti ya kufurahia kazi zetu katika kipindi hiki
ambacho kila mmoja anataka kuonyesha makali yake,” alisema Choki.
Garden Breeze
ukumbi uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam ndio sehemu inayojaza watu wengi
katika burudani za mwisho wa wiki, jambo linalowafanya watu kupata nafasi ya
kuburudika na kazi nzuri za Extra Bongo.
No comments:
Post a Comment