Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Washiriki
wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13,jana
wametembelea Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na wa aina yake Tanzania ambao
unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kurugenzi ya mambo ya kale
na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya Makumbusho ya Taifa jirani na Chuo cha
Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo ya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakiwa
katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja, walishuhudia
Viti,Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa kuendesha Matamasha na
mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya nyota tano.
Mkao huu je?Umeona ehee
Washiriki wa Miss Utalii wakiachia Makumbusho kwa raha zao.
Wengi
wa washiriki hao walionyesha hamasa na kujaribu kuwashawishi viongozi na wakuu
wa msafara wao ili kufanya Fainali hizo katika Ukumbi huo ambao umekuwa ni
kivutio kikubwa, jambo ambalo Viongozi na kamati iliokuwa na jopo la msafara
huo lilionekana kukubaliana na mawazo ya nia ya warembo hao ya kuomba Fainali
hizo zifanyike ndani ya Ukumbi huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo nchini na
Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo,kuhusu uwezekano wa kuandaa Fainali hizo
katika Ukumbi huo wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM THEATRE, alisema
kuwa kila jambo ni mipango, hivyo na kwa kuwa lengo na nia ya Mashindano ya
Miss Utalii ni kutangaza Vivutio vya Taifa kuna uwezekano pia Fainali hizo
zikafanyika hapo ikiwa pia ni kuwapa heshima Wizara ya Maliasili na Utalii
ambao ndiyo walezi wakuu wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania kwa kuwa wao
ndiyo wamiliki wa Ukumbi huo ambao kwa sasa unaonekana kuwa ni kati ya kumbi
pekee zilizojengwa kisasa na hadhi ya kimataifa hapa nchini Tanzania.
Ziara
hiyo ya kutembelea Ukumbi huo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania
2012/2013 iliandaliwa na Washiriki wenyewe baada ya kuusikia sifa zake kutoka
kwa watu mbalimbali na Mitandao ya Kijamii.
Aidha
Chipungahelo amesema kwamba warembo hao wanatarajia kupanda katika jukwaani
baada ya kutoka kwenye ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa ambazo ni pamoja na
Saadan, Mikumi, Udzungwa, Mkomanzi, Arusha na Mlima Kilimanjaro watakaokuwa
wameambatana na waandishi wa habari.
Akizungumzia
hali ya Ukumbi huo Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo
amesema kwamba ni heshima kubwa kwa Taifa na sekta nzima ya Utalii kuona
Warembo ambao wanatangaza Utalii wa Nchi yetu wakivutiwa na ukumbi huo
hata kufikia kupeleka maombi ya kutaka wao kuwa Warembo wa kwanza kupanda
katika jukwaa hilo la Ukumbi wa kisasa na wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM
THEATRE ulipo ndani ya Makumbusho ya Taifa ambao ni kivutio kikubwa kwa sasa
katika anga za Burudani na sanaa.
“Ukumbi
ni mzuri kama ambavyo wenyewe wandishi mlivyoona na kutazama, hakika ni jambo
la kujivunia na kusifiwa kwa Wizara yetu, maana unaonekana ni jambo la
kujipanga hadi kuweza kutengeneza kwa ubora huo unaoonekana sasa, bila shaka
nyie wenyewe mtaona ni kwa kiasi gani Umeandaliwa, lakini hata hivyo ni
changamoto kwa Wizara zingine katika kubuni na kuweka rasilimali kama
hizi kwa manufaa ya Taifa, kama ambavyo mnaona wenyewe, kwani hata Washiriki
wamefurahi na hata kusifia sana hivyo pia nachukua fulsa hii kuishukuru Wizara
kwa kuwekeza Ukumbi wa Kisasa ambao ni faida kwa Taifa” alisema Chipungahelo.
Pia
aliendelea kusisitiza na kuomba wadau na wapenzi mbalimbali wa mashindano haya
kujitokeza kuunga mkono kudhamini na kununua tiketi siku ya shindano..
Erasto
G. Chipungahelo
Rais
– Miss Tourism tanzania Organisation
No comments:
Post a Comment