Uhuru Kenyatta
Na Mwandishi Wetu, Kenya
UCHAGUZI Mkuu Kenya, uliofanyika juzi, umeingia katika sura
mpya, baada ya mtambo wa kuhesabia kura kuendelea kusumbua, hivyo kulazimika
Tume Huru ya Uchaguzi huo nchini hapa kuagiza utaratibu wa kuhesabu kwa mkono
kuanza.
Raila Odinga
Hata hivyo, matokeo yanaendelea kuwa juu kwa mgombea Uhuru
Kenyatta, akiafutiwa na Raila Odinga, mgombea ambaye kwa Tanzania, watu wengi
wameonekana kumuunga mkono.
Tume Huru ya Uchaguzi nchini hapa, iliagiza kura zihesabiwe
kwa mkono katika vituo vya uchaguzi na kuletwa hapa Bomas of Kenya, sehemu
ambayo imeweka Makao Makuu ya muda.
Mtambo huo ulianza kukorofisha tangu jana ambapo
ilisababisha kuhesabu moja kwa moja kushindikana, jambo ambalo huenda likawa
changamoto kubwa katika uchaguzi huu.
Tangu watangaze rasmi kwamba kura zitahesabiwa kwa mkono
mida ya saa saba ni majimbo matatu tu ambayo matokeo yake yametoka mpaka sasa.
Katika hali ya kuongeza msisimko katika Uchaguzi huo hapa
nchini, Wakenya waliopiga kura katika nchi za Afrika Mashariki wamemchagua Odinga
kwa Kura 1224, wakati Kenyata amepata kura 951.
No comments:
Post a Comment