Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
MABINGWA watetezi wa
Ligi ya Tanzania Bara, Simba SC, leo ingia uwanjani kumenyana na timu ya Kagera
Sugar, katika Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu
na mashabiki mkoani Kagera.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga
Mbali na timu ya Simba
kumenyana na Kagera Sugar, mechi nyingine inayochezwa leo ni kati ya Azam na
Prisons ya Mbeya, itakayopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamaz.
Simba wanaingia uwanjani
huku wakiwa na uchu wa kushinda ili wasiendelee kujiondoa katika kushika nafasi
mbili za juu, huku Ligi hiyo ikiongozwa na timu ya Yanga ikiwa kileleni kwa
pointi 48, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 37.
Mabingwa hao watetezi,
Simba, wameondoka jijini Dar es Salaam
kwa mafungu, baada ya wachezaji wake wanaopiga kwenye timu zao za Taifa kufuata
nyuma baada ya kumaliza kwa mechi zao.
Msemaji wa Simba,
Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa wamewaomba washabiki na wanachama wote kuvunja
makundi yao na kuangalia mechi hizo zilizosalia kwa ajili ya kuisaidia klabu
yao.
Kamwaga alisema lengo
lao kubwa ni kushinda mbele ya Kagera Sugar ili wanyakuwe pointi tatu na
kufikisha 37 na kujiweka katika nafasi nzuri katika muendelezo wa ligi hiyo.
“Tunaomba wanachama na
mashabiki wa Simba kuendelea kuwa kitu kimoja juu ya mechi hizi, ukizingatia ni
michezo migumu iliyobaki kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hatubaki nyuma zaidi,”
alisema Kamwaga.
Aidha, katika mchezo awa
Azam na Prisons ya Mbeya, mashabiki watakuwa na shauku ya kuona timu hiyo
iliyoanzishwa kwa malengo makubwa, Azam inavuna nini kutokana na soka lake la
uhakika inaloonyesha.
Azam watakuwa na hamu kubwa ya kushinda katika mechi yao ya
leo, ili ifikishe pointi 40 na kujiweka katika
nafasi nzuri ya kuliwania taji hilo linaloshikiliwa na Simba.
No comments:
Post a Comment