Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya Korogwe |
Na Kambi Mbwana,
Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya Korogwe, Mrisho Gambo, amesema hawawezi
kuchekea vitendo vya ushirikina vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wilayani
kwake, kwa kuita waganga, kutoa uchawi bila mpango.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Gambo alisema vitendo
vya ushirikina havina nafasi, maana wanaofanya hivyo ni wale waliokata tamaa na
maisha, kwa kuona kuna wanaowatia umasikini.
Gambo alisema serikali haiamini ushirikina kama isivyoamini
dini kutoka kwa wananchi wake, hivyo lambalamba anayefanya kazi zake bila
mpango, anastahili kufikishwa mahakamani.
“Kuna walioita waganga bila mpang0, lakini ikumbukwe kuwa
serikali haina dini wala haina imani za ushirikina, hivyo yoyote anayefanya
mambo kinyume atafikishwa mahakamani.
“Hatutaki mambo hayo ya ushirikina katika utendaji wetu wa
serikali, maana mara kwa mara waganga hao huchochea vurugu na kuwafanya watu
washindwe kuishi kwa ushirikiano,” alisema Gambo.
Maneno ya Gambo yamekuja siku moja baada ya wilayani kwake
kutokea vurugu kubwa, wananchi wakilazimisha kuachiwa kwa waganga waliokuwa
wakitoa uchawi kushikiliwa na polisi.
No comments:
Post a Comment