Na
Mwandishi Wetu, Kenya
WAKATI
matokeo yakiendelea kupatikana kwa Uhuru Kenyatta kuongoza kwa kura 2,660,379,
akifuatiwa na Raila Odinga, aliyepata kura 1,996,181, upande wa Odinga umetaka shughuli za uhesabuji
wa kura kusitishwa katika Ukumbi wa Bomas.
Uhuru
Kenyatta angali anaongoza kwa idadi ya kura za wagombea wa urais akiwa na kura
2,660,379 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliye na kura 1,996,181 lakini
matokeo rasmi yatajulikana tu mwishoni mwa juma.
Habari
hizo zimeubua hisia na wasiwasi katika Uchaguzi huo nchini hapa, ikiwa ni
matokeo magumu yanayoweza kuleta mtafaruku miongoni mwa Wakenya.
Hatua
hii imelazimu tume hiyo kuanza kuhesabu kura upya katika kitovu cha kupokea
matokeo ya kura za urais kwenye ukumbi wa Bomas viungani wa mji wa Nairobi.
Kalonzo
Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Raila Odinga, amehutubia waandishi wa
habari mjini Nairobi na kusema kuwa muungano wa CORD, unataka shughuli hiyo ya
kuhesabu kura za urais kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya wakitumia stakabadhi
kutoka kwa makarani wa kura jambao ambalo linafanywa kwa sasa
Aliendelea
kwa kusema kuwa baadhi ya matokeo yako juu kuliko idadi ya wapiga kura katika
baadhi ya maeneo ambako kura zilipigwa, huku akisema kuwa tatizo hilo
limetokana na kugoma kwa mitambo ya kupiga kura.
No comments:
Post a Comment