Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu.
Ofisa Elimu wa Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Stori, picha kwa hisani ya Joachim Mushi.
MATUKIO
ya kesi za kuwatia mimba/kuwabaka wanafunzi yaliokuwa yameshamiri
katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Handeni sasa
yameanza kupungua tofauti na ilivyokuwa awali. Kwa mujibu wa uchunguzi
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa kushirikiana na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 na Machi 2013
matukio ya mimba yanapungua.
Akizungumzia
hali hiyo juzi Wilayani Handeni, Ofisa Elimu wa Wilaya, Mgaza Muchiwa
alisema matukio ya mimba kwa wanafunzi yanapungua tofauti na miaka ya
nyuma ambapo matukio ya utoro wa mimba kwa wanafunzi yalikuwa mengi.
“Picha ya mwaka jana niliiona na tulikuwa tukifuatilia kwa karibu matukio ya kesi za mimba kwa wanafunzi…huwezi kufananisha na ilivyo sasa kunamabadiliko kwani matukio haya yamepungua,” alisema Muchiwa akizungumza na mwandishi ofisini kwake Handeni juzi.
“Picha ya mwaka jana niliiona na tulikuwa tukifuatilia kwa karibu matukio ya kesi za mimba kwa wanafunzi…huwezi kufananisha na ilivyo sasa kunamabadiliko kwani matukio haya yamepungua,” alisema Muchiwa akizungumza na mwandishi ofisini kwake Handeni juzi.
Mkuu
wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera alithibitisha pia kupungua
kwa kesi za mimba zinazofikishwa katika vituo vya Polisi ukilinganisha
na hapo nyuma. Akifafanua zaidi kupitia taarifa za Dawati la Jinsia na
Watoto Kituo cha Handeni, alisema hadi Novemba 2012 walipokea kesi 66 za
matukio hayo lakini tangu hapo hadi Machi mwaka huu kesi hizo
zimepungua kwa kiasi kikubwa.
Uchunguzi
uliofanywa na www.thehabari hivi karibuni katika shule za sekondari
Komnyang’anyo, Kileleni na Kivesa zote za wilayani Handeni umeonesha
kupungua kwa matukio ya mimba kwa wanafunzi, huku walimu wakidai hali
hiyo imechangiwa na kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa
Wilaya mpya, Muhingo Rweyemamu.
“Kweli
kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya
imesaidia sana maana watu wameanza kuogopa kuwarubuni wanafunzi…hata
wazazi na wanafunzi nao wanaogopa kuhusishwa katika kesi hizo hii
imesaidia kupunguza matukio ya mimba,” alisema Kaimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari Komnyang’anyo Nadhiru Kinyama.
Mkuu
wa Wilaya hiyo, Rweyemamu Agosti 2012 alianzisha kampeni ya kupambana
na watu waliyokuwa wakiwakatisha masomo wanafunzi kwa kuwatia mimba na
kuwaozesha kwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja
na kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii juu ya umuhimu wa elimu wilayani
humo.
No comments:
Post a Comment