https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, March 19, 2013

Uongozi Simba waendelea kujificha kwenye kivuli cha TFF

Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua kutoka uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.

Hata hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...