Mrisho Gambo, Mkuu wa wilaya ya Korogwe
Na Mwandishi Wetu, Korogwe
HALI ni mbaya kwa wilaya ya
Korogwe na Handeni kutokana na vijana wengi kujiingiza kwenye dhahma ya kuita
waganga wa kutoa wachawi, maarufu kama lambalamba bila kufuata utaratibu na kuzua hofu.
Mkuu wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Leo, katika mji wa Korogwe,
polisi wamelazimika kutumia nguvu kubwa kutuliza ghasia kutoka kwa vijana
waliokuwa wanapinga mganga wao kukamatwa na kusekwa lupango.
Polisi hao walimkamata mganga
huyo baada ya kutoa vitu vinavyodaiwa ni uchawi kutoka kwa mtu anayefanya kazi
ya kukatisha tiketi katika stendi ya mabasi ya Korogwe, jina lake
linahifadhiwa.
Shuhuda wetu aliyekuwa mjini
Korogwe, aliiambia Handeni Kwetu kuwa juhudi za polisi kuzuia mganga huyo
asiendelee na kazi yake zimesababisha mgogoro na wananchi.
Hapa Korogwe kuna uchawi sana,
lakini kwakuwa serikali haiamini uchawi basi wananchi tunaendelea kutumika
vibaya, ndio maana hata hao waliotolewa uchawi huo wanalalamikiwa sana.
Suala hili limewafanya baadhi
ya watu washindwe kujuzuia na kuzua mjadala kutoka kwa jeshi la polisi juu ya
oparesheni hii ya kutoa uchawi katika maeneo ya mji huu,” alisema mdau huyo.
Juhuzi za kufanya mazungumzo na
Kamanda wa Polisi za Wilaya na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mrisho Gambo zinaendelea
juu ya sakata hilo linalosumbua kwa wiki kadhaa sasa.
Naye Mkuu wa Wilaya Handeni,
Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa wilaya yake imezidi kukumbwa na suala hilo la
lambalamba, katika vijiji mbalimbali.
Tumekubaliana kuwa mgogoro kama
huu unapotokea, anakamatwa mganga huyo,” alisema Muhingo.
Katika kijiji cha Komsala,
wilayani Handeni mkoani Tanga, lilijitokeza suala hilo Ijumaa iliyopita na
kulazimika polisi kuvamia na kuwakamata watu mbalimbali ambao hata hivyo
baadaye waliachiwa baada ya zogo hilo kumalizika na shughuli za kijamii
kuendelea.
No comments:
Post a Comment