Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NIMEKUWA nikifuatilia na
kukoshwa na mwendo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, hasa katika upande wa kuunga mkono sanaa na wasanii hapa nchini.
Mara kwa mara Rais Kikwete
amekuwa akitoa kwa moyo wote kuwaunga mkono wasanii, jambo ambalo hakika
halitasahauliwa na watu wote, hasa wale wanaofuatilia sanaa Tanzania.
Hapo kipindi cha nyuma, ilikuwa
ni ngumu kumuona rais anakuwa kwenye sehemu ya jamii zote, ukizingatia kuwa
katika kipindi cha utawala wa marais waliotangulia, akiwamo Benjamin Mkapa,
Rais Ali Hassan Mwinyi, sanaa iliitwa ni uhuni.
Si ajabu nao waliogopa kuitwa
wahuni, ndio maana uwepo wao haukuwa na tija sana, ingawa wasanii waliendelea kuwa
na upendo na nchi yao, hasa kwa kuona wanaendelea kutunga nyimbo nzuri au
filamu za kuelimisha jamii kwa ajili ya kukuza uchimi wan chi yao.
Katika kulisema hilo, nachukua
fursa hii kushukuru juhudi za Rais Kikwete, huku nikiamini kuwa mwarobaini wa kilio
cha wasanii anao yeye, kama amri jeshi mkuu wa Tanzania.
Yeye ndio kila kitu. Hakuna
analoweza kusema yeye na likapingwa, hasa kaatika nchi hii inayojiendesha kwa
utawala wa sheria. Hivi karibuni, nilipata kuzungumza na Rais wa Shirikisho la
Muziki Tanzania, Ado Novemba.
November alizungumza mengi,
lakini kubwa zaidi alionekana kupokea maneno kutoka kwa Rais Kikwete, kuwa
anaendelea na juhudi zake kuhakikisha kuwa utawala wake unakuwa na tunu kwa
wasanii.
Maneno yake yamekuja huku
akisema kuwa ili aweze kufanikisha suala hilo, atawaagiza Shirika la Posta,
kulivalia njuga suala la usambazaji wa kazi za wasanii ili zipatikane nchi
nzima.
Kabla Posta kupewa jukumu hilo,
kazi za wasanii zilikuwa zinapatikana kwa tab u mno katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania. Leo hii msanii Ahmad Allly Madee, Profesa Jay, Juma Nature kwa upande
wa Bongo Fleva, wanaweza kuwa na mashabiki katika wilaya au mikoa husika,
lakini wadau hao wasipate fura ya kununua kazi zao.
Hii ni kwasabu zinapatikana kwa
ugumu mno. Kubwa shabiki huyo analoweza kufanya ni kuchoma katika vipanda hasa
maeneo ya mijini, kama njia za kumuwezesha kusikiliza nyimbo hizo.
Huu ni wizi wa aina yake. Kwa
bahati mbaya, wizi huu unachochewa kwa kiasi kikubwa na mfumo mzima wa Taifa
letu. Hakuna msambazaji mkubwa zaidi ya hawa ambao kwa miaka mingi
wanalalamikiwa.
Waandaaji wa filamu wanalia
kila siku. Kazi zao hazisambai kwa wakati, hivyo kuchochea ugumu wa maisha yao.
Huu ndio ukweli wa mambo. Na katika kulijua hilo, naamini kuwa Rais Kikwete kwa
utashi wake, mapenzi yake kwa wasanii wa Tanzania, hakika anaweza kulipatia
ufumbuzi suala hilo.
Na upendo huo wa JK kwa wasanii
wa Tanzania, unaweza kuja kwa sababu kuu mbili. Mosi, JK amesaidiwa sana na
wasanii wa Tanzania. Kwa mfano, katika kampenzi za mwaka 2005, yeye akiwa
mgombea kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wasanii walifanya kazi kubwa
mno.
Wasanii kibao walifanya kazi
kwa mapenzi mema na Kikwete. Wanaume Family, akiwa Juma Nature na wenzake
walifikia kutunga nyimbo na vibwagizo vya aina yake kwa ajili ya kuonyesha
mapenzi kwa JK.
Msanii kama Bushoke, wadau
wanakumbuka jinsi alivyougeuza wimbo wake wa Mume Bwege na kutaja jina la
JK na CCM kwa nguvu kubwa mno. Pamoja na
hao, bado kulikuwa na mtiririko wa safari na ziara za wasanii kwenye kampeni
ambazo baadaye alishinda urais kwa kishindo.
Ukiacha kampeni za mwaka 2005,
mwaka 2010 pia wasanii lukuki walifanya kazi za maana kwa ziara za CCM. Wasanii
kama vile Diamond, Marlaw na wakali wengine walipishana katika barabara
wakitaja jina la JK na CCM kwa nguvu zote, hali iliyochangia mafanikio yake.
Hakika kwa kulisema hilo, basi
ndio maana hata JK mwenyewe amekuwa na mapenzi na wasanii wa Tanzania, hivyo
katika suala kama hili, lazima alivalie njuga kitu chochote kinachohusu sanaa
na wasanii.
Sina nia mbaya ya kumshurutisha
Rais Kikwete, ila kauli yangu inakuja kwasababu tayari ameonyesha nia ya dhati
ya kutetea maisha ya wasanii wanaoendelea kufa kwa njaa licha ya kuwa na kazi
nzuri.
Rais Kikwete anajua kuwa
ukiacha kujulikana kwa vijana hawa, bado hawana kitu cha kujivunia katika mitaa
yao. Wengi wao bado wanaishi kwa virungu, kuomba msaada kutoka kwa wadau wao.
Ni wachache wanaojimudu
kimaisha, huku kujimudu huko kukiwa kwa siku chache, kabla ya kupotea kwa muda
mrefu. Wapo wasanii ambao miaka ya 2010 walikuwa wanajiweza kiuchumi, lakini
leo hii hawana kitu.
Hiyo imesababishwa na mfumo
wetu mbovu. Wasanii kuneemeka kwa siku mbili au tatu, hasa pale anapopata shoo
zinazolipwa kwa fedha ndogo kutoka kwa wadau wanaoshiba jasho la wasanii.
Huu ndio ukweli. JK anapaswa
kulifanyia kazi suala hili kama mwenyewe alivyoonyesha nia hiyo kwa ajili ya
maendeleo ya wasanii wa Tanzania, kama njia za kuwabeba na kuwaweka pazuri.
Ndio, Rais Kikwete ametangaza
kuwa, katika kipindi cha utawala wake, atahakikisha kuwa maisha ya w asanii
yanakuwa juu katika hali ya kuifanya sekta ya sanaa kuwa juu.
Huu ndio ukweli wa mambo.
Nauzungumza kama mdau wa sanaa, ambaye muda mwingi nimekuwa nikiangalia kwa
karibu sekta ya sanaa na matatizo yake yanayowakabiri kwa namna moja ama
nyingine.
JK yeye ndio mwarobaini wa
kelele zinazopigwa na wasanii wetu, hasa hizi za kutokuwa na imani na vyombo
vya serikali vinavyohusiana na mambo ya sanaa, kikiwamo kile cha COSOTA,
ambacho kwa hakika kila msanii anakilalamikia kwa kushindwa kuweka mipango imara.
Ndio hapo sauti ya rais
itakavyokuwa na mgusos, atakapoagiza lazima stika za kuwekwa kwenye kazi
ziwekewe utaratibu mzuri, zisifanane, kila mmoja iwe na nembo yake kwa ajili ya
kuepusha wizi na migogoro.
Pamoja na mambo mengine,
lakaini serikali ikifanyia kazi na kulipatia ufumbuzi suala hili, hakika hata
mapato ya wasanii yataongezeka pamoja na kutoa fursa ya kodi kuingia serikalini
kwa utaratibu maalum.
Hakika, katika hili, napongeza
na kutambua juhudi za Rais Kikwete, huku nikiamini kuwa anaweza kufanya
palipokuwa na giza kukawa na mwanga, hasa katika suala zima lisilomuhusisha
Mwenyezimungu.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment