Ukosefu wa walimu, upungufu
wa vitabu na mazingira duni ya kujifunzia, ni baadhi ya sababu zilizotolewa kwa
wingi na wadau wa elimu waliohojiwa na Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha
Nne mwaka 2012 iliyoundwa na Waziri Mkuu.
Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa tume hiyo, Profesa Sifuni Mchome alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Profesa Mchome
alitaja sababu nyingine zinazotolewa kuwa ni pamoja na shule nyingi kutokuwa na
mabweni pamoja na miundombinu mibovu ya kujifunzia.
No comments:
Post a Comment