Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars wakishangilia
Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16
mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya
Morocco.
Mechi hiyo ya mchujo
kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani
nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Kocha Kim,
wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa
kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni
makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula
(Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey
Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani
(Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe
(Simba).
Viungo ni Salum Abubakar
(Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank
Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John
Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC),
Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la
ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa
timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
No comments:
Post a Comment