Ridhiwani Kikwete
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Jengo la Mafia la Klabu ya Yanga, Ridhiwani Kikwete, amesema kwamba wataiabisha Simba kwa
kuhakikisha kuwa wanaiweka klabu yao katika nembo ya kibiashara na mafanikio
lukuki.
Ridhiwani aliyasema hayo mapema
wiki hii, mara baada ya kuteuliwa na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuwa
mwenyekiti wa kamati hiyo sambamba na kumpa mamlaka ya kuteua watu anaotaka
kufanya nao kazi kwenye kamati hiyo.
Akizungumza mapema wiki hii, Ridhiwani alisema kwamba hawaitaji kupiga soga katika mambo ya
kimaendeleo, hivyo wadau wa Simba wajiangalie mara mbili.
Alisema lengo kubwa ni
kuhakikisha kuwa kila mtu anafanya mambo yenye maendeleo na Yanga, hivyo wenye
mapenzi mema na klabu yao ni wakati wa kushirikiana na kusubiri mafanikio yao.
“Wale ndugu zetu wa upande wa
pili, Simba SC wajiandaye pia kusubiria mafanikio kutoka kwetu, maana tutafanya
kazi kwa moyo na mapinduzi makubwa nchini.
“Huu ni wakati kuiweka Yanga
kwenye kilele cha mafanikio na sio kupiga porojo, hivyo naamini mambo yatakuwa
mazuri na hakika watu wataishia kuchungulia mafanikio kutoka kwetu,” alisema.
Kamati ya Ridhiwani itahusika na
kupitia na kuratibu ujenzi wa jingo la Mafia, Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kuhakikisha kuwa klabu yao inajiendesha kibiashara.
No comments:
Post a Comment