MPAMBANO uliokuwa unangojewa kwa hamu na watu wengi wa kumpata Mfalme
wa uzito wa bantam wa kimataifa kati ya mabondia Immenuel Naidjala a.k.a Prince
kutoka Namibia na Lesley Sekotswe kutoka Botswana haukuweza kutoa mshindi baada
ya matokeo ya majaji wawili kumpa kila mmoja ushindi wan a jaji wa tatu kutoa
droo.
Pambano hili lilikuwa limeandaliwa na kampuni ya Sunshine
Promotions ya bwana Nestor Tobias na lilikuwa na kila aina ya hamasa baada ya
mabondia wote wawili kuonyesha ufundi wa kurusha makonde.
Rais wa IBF kutoka Afrika, Ghuba ya Uajemi na mashariki ya
Kati Mtanzania Onesmo Ngowi ambeye alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa mpambani huu
alitangaza kuwa mabondia wote wawili watakutana tena baada ya kipindi cha
mapumziko ya mwezi mmoja ili kuweza kumpata mshindi wa mkanda huo ambaoni
watatu kwa umaarufu katika mukanda ya ngumi.
Mkanda wa kwanza kwa umaarufu ni
wa ubingwa wa dunia. Mkanda wa tatu ni wa ubingwa wa mabara na mkanda wa tatu
ni wa ubingwa wa kimataifa ambao ndio uliokuwa unagombewa na mabanodia hao.
Wakazi wengi wa jiji la Widhoek na miji mingine ya jirani
pamoja nan chi za jirani walijazana katika hotel ya Widhoek Country Club and
Casino kuushughudia mpambani huo ambao ulikuwa na kila aina ya hamasa.
No comments:
Post a Comment