KAMPUNI ya QS Entertainment, imeandaa tamasha kubwa la ‘Tumaini
Jipya’ linalotarajiwa kufanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro likihusisha waimbaji
mbalimbali hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya QS Entertainment, Joseph
Mhonda alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwasaidia watu wenye
mahitaji maalumu kwenye jamii ikiwemo
watoto yatima na kutarajiwa pia kufanyika katika mikoa mbalimbali baada ya
kuzinduliwa mkoani Morogoro likiwa na lengo kubwa la kueneza neno la bwana na mambo mengine ya kijamii katika kila mkoa watakapokuwapo.
Martha Mwaipaja akizungumza
jambo na mwimbaji mwingine wa muziki wa Injili, Stara Thomas, aliyewahi kuwika
pia kwenye muziki wa Kidunia, maarufu kama Bongo Fleva.
Martha Mwaipaja,
akizungumza jambo.
Mkurugenzi wa Kampuni
hiyo, Joseph Mhonda, ambao ndio waandaaji wa tamasha akiwa mbele ya kamera ya Handeni Kwetu Blog.
Mkurugenzi wa Kampuni
hiyo, Joseph Mhonda, katikati akizungumzia uzinduzi wa tamasha hilo la Tumaini Jipya.
Stara Thomas akiwa na wakali wengine wa muziki wa Injili Tanzania.
Mwimbaji wa muziki wa Injili, Stara Thomas,
akisikiliza kwa umakini utambulisho wa tamasha la Tumaini Jipya linalotarajiwa
kufanyika Machi 31, katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku likiandaliwa
na Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment.
No comments:
Post a Comment