Mgombea Urais Kenya, Raila Odinga
Na BBC, Swahili
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya imekiri kuwa kulikuwa na
hitilafu chungu nzima za kimitambo, katika kutoa matangazo ya matokeo ya kura
za urais kutoka kwa vituo vya kupigia kura kote nchini.
Afisaa mkuu mtendaji
wa tume hiyo, James Oswago alielezea kuwa hitilafu hiyo ilisababishwa na kiasi
kikubwa cha matokeo yaliyokuwa yanapeperushwa moja kwa moja kutoka kwa vituo
vya kupigia kura kwa sababu ya ukosefu wa nafasi ya kutosha kwenye mitambo
yake.
Akihutubia
waandishi wa habari katika ukumbi wa Bomas ambako matokeo ya urais yanatarajiwa
kutangazwa, Bwana oswago alisema kuwa tume hiyo iliweza kurekebisha mitambo
yake.
Pia aliongeza kuwa
maajenti wa wagombea wote wakuu wawili walifahamishwa kuhusu hutilafu hiyo.
Kugoma kwa muda kwa
mitambo ya kupeperusha matokeo, ilisababisha hali ya wasiwasi, baada ya IEBC
kusitisha kupeperusha matangazo kwa masaa kadhaa.
Maafisa wa Miungano
yote ya Jubiliee na CORD, walitetea kwa sababu ya kucheleweshwa kwa matokeo na
kulaumu tume ya IEBC, baada ya maafisa wake wote kuondoka katika ukumbi wa
kutangazia matokeo ya urais.
Kamishna mmoja mkuu
wa tume hiyo aliwataka watu kuwa watulivu akisema hakuna sababu ya watu kuwa na
wasiwasi.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment