Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa
akiwakaribisha walimu wapya
|
Na Mwandishi Wetu, Kilwa
JUMLA ya walimu wapya 152 wa shule za Msingi
na Sekondari wameripoti wilayani Kilwa kati ya walimu 182 waliopangwa
kufundisha Wilayani humo. Akizungumza kwenye mkutano na walimu hao Mkuu wa
Wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega alisema walimu walipangiwa kufundiosha Wilayani
humo walikuwa ni 182 kati ya hao 104 wa Shule za Msingi na 78 wa Sekondari.
Aidha Ulega alifafanua kuwa walimu wasioripoti licha ya
muda wakufanya hivyo kumalizika ni 7 wa Shule za Msingi na 23 wa Sekondari.
Tukio hilo la kuwapokea walimu hao limekwenda sambamba na makabidhiyano ya meza
nne za maabara inayotembea kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa ni sehemu
ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari za
wilaya hiyo Hususan katika masomo ya sayansi.
Mkuu huyo wa Wilaya mbali na kuwashukuru walimu hao kwa
kufika wilayani humo.
Pia alitoa wito kwa Jamii kujenga Nyumba Bora hususan Vijijini ili kusaidia
watumishi wanaopangwa huko kwa huduma za jamii zikiwemo Elimu na Afya kutokana
na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa
zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi licha ya kuwawezesha wanafunzi sasa
kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Bw
Addo Mapunda aliwasihi
walimu hao kufanya kazi kwa kuwa Wilaya hiyo inaupungufu mkubwa wa walimu
hususan vijijini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw Ally Mohamed Mtopa alitoa
ahadi ya kununua kitanda na godoro kwa walimu watakaopangwa katika kata yake
lakini pia aliwageukia walimu hao kuhusiana na suala la migomo ya walimu ambapo
aliwasihi kutojiingiza katika masuala hayo badala yake aliwaomba walimu hao kufikisha malalamiko yao kwa Madiwani ambao
ndio wenye maamuzi ya Halmashauri hiyo
|
No comments:
Post a Comment