https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, March 01, 2013

Mbwana Matumla asifia viwango cha Kaseba, Oswald

Mbwana Matumla akiwa ulingoni.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mbwana Matumla, amesema pambano la Japhet Kaseba na mpinzani wake Maneno Oswald, litakuwa zuri kutokana na umahiri wa wakali hao wa masumbwi hapa nchini.
Mabondia hao wanatarajia kuzipiga Machi mbili katika Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa, jijini Dar es Salaam, huku mgeni rasmi akiwa ni Kamanda wa Polisi KanDA Maalum ya Dar es Salaam, Selemani Kova.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Matumla alisema Kaseba na Osward ni mabondia mahiri katika ngumi nchini, hivyo mpambano wao utakuwa wa aina yake.
Alisema kwamba anaamini mashabiki watapata kitu kizuri kutoka kwa mabondia hao, maana ni hodari wa kurusha masumbwi pamoja na uzoefu wa aina yake.
“Pambano la Kaseba na Oswald litakuwa la aina yake, maana ni mabondia mahiri na wenye uwezo mzuri, hivyo naamini upinzani utakuwapo kwa wawili hao ulingoni.
“Wamekuwa kwenye mvutano wa siku kadhaa tangu kutangazwa kwa pambano hilo, katika suala zima la masumbwi, lolote linaweza kutokea, hivyo tusubiri tupate majibu,” alisema.
Kuelekea kwenye pambano hilo la Osward na Kaseba, kumekuwa na tambo za aina yake kutoka kwa wawili hao, huku kila mmoja akijigamba kumtandika mwenzake.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...